Kikosi cha Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara Simba SC, mapema hii leo kiliwasili jijini Dar es salaam kikitokea Mkoani Lindi kupitia Mtwara ambapo walikuwa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo.

Mchezo huo uliochezwa jana Jumatano, kikosi cha Simba SC kiliambulia matokeo ya sare ya bila kufungana, na baada ya mchezo huo wachezaji walikabidhiwa medali pamoja na kupewa kombe la ubingwa.

Kombe hilo la ubingwa linakuwa la kwao jumla, kwa kuwa wametwaa mara tatu mfululizo hivyo kwa mujibu wa kanuni linakuwa mali yao.

Hilo linakuwa taji la 21 la Ligi Kuu kwa Simba SC baada ya awali kubeba taji hilo mwaka 1965, 1966, 1973, 1976, 1977, 1978, 1979, 1980, 1984, 1990, 1994, 1995, 2001, 2003, 2004, 2007 (Ligi Ndogo), 2010, 2012, 2018 na 2019.

Baada ya kuwasili uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kikosi cha Simba kilisindikizwa na mashabiki na wanachama wao kuelekea makao makuu ya Simba, Msimbazi.

Stones kujihukumu mbele ya bosi
Salamu za pongezi zamiminika Simba SC