Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa amewataka wananchi wa Mkoa wa Tabora kuacha mara moja kuendeleza ujenzi na kilimo kwenye hifadhi ya barabara wakati serikali imeshatumia fedha nyingi kulipa fidia ili kupisha ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami.

Amesema kuwa serikali inatumia zaidi ya shilingi bilioni 894 kutekeleza miradi mikubwa minne ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami zenye urefu wa zaidi ya kilomita 500 Mkoani Tabora.

“Miundombinu ya barabara ndio kiungo muhimu katika ukuaji wa uchumi wa nchi yoyote hivyo wananchi mnapaswa kuwa walinzi wa utunzaji wa barabara hizo,”amesema Prof. Mbarawa

Hata hivyo, Prof. Mbarawa amesema kuwa wakazi wote ambao watakua wameingia katika maeneo ya barabara hawatalipwa fidia yoyote na kuwataka waondoke haraka huku akisema serikali haitasita kuwalipa wale wote watakaopisha ujenzi wa barabara kwa mujibu wa sheria.

Watu 250 wauawa ndani ya saa 48
Video: Milioni 80 kumzika Akwilina, Makubwa yafichuka kwa Kakobe