Kwa mara ya kwanza baada ya mvutano wa muda mrefu Bungeni kati ya wabunge wa vyama vya Ukawa na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson wamekutana jana katika makabidhiano ya madawati yaliyotokana na fedha zilizotolewa na Bunge kwa Rais kutokana na kubana matumizi.

Rais John Magufuli alikuwa mgeni rasmi katika tukio hilo la maendeleo lililofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, ambapo wabunge wa Ukawa, Mchungaji Peter Msigwa (Chadema) na Magdalena Sakaya (CUF) ambao ni wajumbe wa Tume ya Huduma za Bunge iliyoratibu utoaji madawati hayo 60,000 walikuwa miongoni mwa wahudhuriaji.

Rais Magufuli alionesha kufurahishwa na uhudhuriaji wa wabunge hao pamoja na Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita ambapo alimpa nafasi kuwasalimu maofisa waandamizi wa majeshi ya ulinzi na usalama waliohudhuria.

“Leo nimefurahi kweli, maana namuona Msigwa pale tumetaniana ‘kamwene anogage’. Nanuona amekaa karibu na Dk. Tulia Ackson (Naibu Spika wa Bunge),” alisema Rais Magufuli na kusisitiza kuwa hiyo ndiyo Tanzania anayoitaka, kuungana katika masuala ya maendeleo bila kujali itikadi ya vyama.

Kadhalika, Rais Magufuli alimsifia Meya wa Jiji la Dar Salaam aliyezungumza machache baada ya kupewa nafasi ya kuwasalu waalikwa. Meya huyo alimpongeza Rais Magufuli kwa juhudi zake na kuongeza kuwa anategemea kuwa baada ya madawati atatoa maagizo ya kuongeza vyumba vya madarasa ili kuondokana na tatizo la msongamano wa wanafunzi.

Rais Magufuli alisema kuwa Meya huyo alitoa maelezo yaliyojaa uzalendo na kuuahidi kumpa nafasi ya uteuzi endapo Chadema watamfukuza kwasababu za kumfia, kwakuwa bado anazo nafasi nyingi.

“Wabunge wa vyama vingine vilivyopo hapa nipo hapa kushirikiana na nyinyi kuleta maendeleo. Maendeleo hayana chama ingawa chama kinachotawala ni CCM,” alisema.

Video: Ni Noma ya Lulu Kuingia Sokoni Rasmi
Haji Manara Apokea Mchango Wa Young Africans