Ikiwa soka la Zanzibar bado hali yake siyo njema kutokana na Migogoro ya wenyewe kwa wenyewe hasa hasa Viongozi wa juu wa chama kinachosimamia mchezo huo visiwani Zanzibar (ZFA) ambao bado wanavutana, Rais wa Kamati ya Olympik Tanzania (TOC) Gulam Abdallah Rashid amewataka ZFA watengeneze katiba inayokwenda na wakati ili isaidie kutatuwa migogoro ambayo si ya lazima.

Gulam aliyasema hayo wakati anafunga Semina ya siku mbili ya Leseni za Vilabu vya Zanzibar iliyoendeshwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika “CAF” yaliofanyika katika Hoteli ya Zanzibar Ocean View iliyopo Kilimani mjini Unguja ambapo Mafunzo hayo walishiriki baadhi ya Viongozi wa ZFA, Makocha na wadau wengine wa mpira wa Miguu.

“ Najua ZFA wapo katika wakati mgumu sasa, lakini nawaomba wakati wa kutengeneza Katiba ya ZFA basi wafate miongozo na utaratibu wa kimataifa zaidi ili migogoro ipunguwe, na naamini yataondoka kama watafata miongozo hiyo, lazima ujuwe Dunia inataka nini kwenye soka , lazima tubadilike”. Alisema Gulam.

Alex McLeish Kocha Mpya Zamalek FC
Donald Ngoma Kuwakosa Mabingwa Wa Mauritius Jumamosi