Mshambuliaji wa Yanga Donald Dombo Ngoma ataukosa mchezo wa kimataifa marudiano kati ya Cercle de Joachim kutokana na kufiwa na mdogoake nchini Zimbabwe.

Taarifa za nyota huyo kufiwa na mdogoake zilimfikia jana usiku na uongozi wa Yanga ukafanya jitihada kuhakikisha mchezaji huyo anaondoka kwenda nyumbani kwao Zimbabwe kwa ajili ya mazishi. Ngoma ameondoka leo alfajiri na anatarajiwa kuungana na kikosi cha Yanga mara baada ya kukamilisha taratibu za msiba.

Wachezaji wengine ambao wataukosa mchezo huo ni Haruna niyonzima ambaye anaumwa pamoja na Salumu Telela ambaye pia ni mgonjwa.

Uongozi wa Yanga umetangaza viingilio vya mchezo wa Jumamosi February 27, kiingilio cha juu kitakuwa ni Tsh. 30,000 wakati kiingilio cha chini kikiwa ni Tsh. 5000. Tiketi zitaanza kuuzwa siku ya Ijumaa 26-02-2016 katika vituo vifuatavyo; Ofisi za TFF (Karume), Makao Makuu ya klabu (Jangwani), Dar Live (Mbagala) na Buguruni.

Kikosi cha Yanga kipo kambini jijini Dar es Salaam kikiendelea kujinoa kwa ajili ya mchezo wao wa Jumamosi.

Raisi Wa TOC Awataka ZFA Watengeneze Katiba Iliyo Bora
SADZ: Wadau Jitokezeni Kutuunga Mkono