Mabingwa wa ligi kuu ya soka nchini England, Leicester City wataanza mkakati wa kutetea ubingwa wao msimu wa 2016-17 kwa kupambana na klabu ya Hull City iliyorejea ligi kuu ikitokea ligi daraja la kwanza.

Mkakati wa mabingwa hao umefahamika muda mchache baada ya chama cha soka nchini England FA, kutangaza ratiba kamili ya msimu ujao wa ligi ambao umepangwa kuanza August 13 mwaka huu.

Katika ratiba hiyo, pia inaonyesha meneja mpya wa Man Utd, Jose Mourinho ataanza kufanya kazi ya kuusaka ubingwa wa Angland akiwa na mashetani wekundu kwa kupambana nan Bournemouth, huku meneja kutoka nchini Hispania Pep Guardiola aliyebeba jukumu la kuwanoa Man City akikabidhiwa mtihani wa kufungua pazia kwa kuchakatana na kikosi cha Sunderland ambacho kinanolewa na Sam Allardyce.

Hii itakua ni mara ya kwanza kwa Guardiola kukaa kwenye benchi la Man City na kuongoza kikosi kinachoshiriki ligi ya nchini England, huku mashabiki wengi wanatarajia kuona uzoefu wake ambao ulimsaidia kutwaa mataji kadhaa akiwa na klabu za FC Barcelona na FC Bayern Munich.

Kimbembe kikubwa katika michezo ya ufunguzi ya ligi ya nchini England, kinatarajiwa kuwa katika uwanja wa Emirates uliopo kaskazini mwa jijini London ambapo Arsenal wataanza kampeni yao kwa kupapatuana na majogoo wa jiji Lverpool.

Meneja wa Chelsea Antonio Conte, atakua na jukumu la kukiongoza kikosi chake katika mchezo wa kwanza utakaochezwa kwenye uwanja wa Stamford Bridge kwa kuwakaribisha majirani zao West Ham.

Naye meneja mpya wa klabu ya Everton, Ronald Koeman ataanza maisha huko Goodson Park kwa kuwakabili Tottenham ambao wananolewa na Mauricio Pochettino aliyemuachia nafasi huko St Maries, wakati akiondoka na kuelekea kaskazini mwa jijini London.

Mchezo huo umepangwa kuchezwa katika uwanja wa klabu ya Everton unaotambulika kwa jina la Goodison Park.

Klabu ya Burnley iliyopanda daraja mwishoni mwa msimu uliopita ikitokea ligi daraja la kwanza itaanza harakati za kusaka taji la England kwa kupambana Swansea Ciy katika uwanja wa nyumbani wa Turf Moore, na wenzao waliopanda daraja Middlesbrough watawakaribisha Stoke City huko Riverside Stadium.

Simba Waendelea Kumsaka Kocha Kimya Kimya
Ndoa Ya Telela Na Young Africans Yafikia Tamati