Mwanafamilia wa lebo ya WCB, Rich Mavoko amezungumzia mafanikio aliyoyapata tangu alipojiunga na lebo hiyo inayomilikiwa na msanii mwenzake, Diamond Platinumz.

Mavoko ambaye ametimiza mwaka mmoja na miezi kadhaa tangu ajiunge na lebo hiyo, amesema ndani ya kipindi hicho kuna mabadiliko makubwa katika muziki wake na kwamba anafaidika zaidi na ongezeko la mashabiki wapya anaoendelea kuwapata kila siku.

Mavoko amesema WCB imesaidia muziki wake kufika mbali na kutambulika zaidi kwenye anga za kimataifa, kitu ambacho ingekuwa vigumu kukifanya kama angekuwa pekee yake kama ilivyokuwa awali.

“Kidole kimoja hakivunji chawa, nisingeweza kufanya vitu vyote peke yangu. Nisingeweza kufika mbali bila kuwa na timu. Lazima niwashukuru watu waliopo nyuma yangu ambao wana-push (wanasukuma) kazi zangu,’’ Mavoko ameiambia Nipe tano ya TBC FM.

Pamoja na mafanikio anayoendelea kuyapata akiwa mwanafamilia wa WCB, Mavoko amekiri kuwa anakumbana na changamoto kadhaa lakini anajitahidi kuzitatua ili azifikie ndoto za mafanikio zaidi katika muziki wake.

Magazeti ya Tanzania leo Agosti 28, 2017
Video: CCM imejipanga kupata viongozi waadilifu- Polepole