Mwenyekiti wa Zamani wa Chama cha soka nchini (FAT) sasa TFF Said Hamad El Maamry amefariki dunia.

El Maamry ambaye alikuwa pia Mwanasheria maarufu aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Michezo BMT, amefariki usiku wa kuamkia leo Hospital ya Taifa Muhimbili.

Tayari familia ya marehemu imeshatangaza taratibu za maziko ya Marehemu mpendwa wao.

RATIBA YA MAZIKO ya ALHAJ SAID HAMAD EL MAAMRY

Jumapili tarehe 25/07/2021

Saa 9:00 Alasir: Mwili wa marehemu ALHAJ SAID HAMAD EL-MAAMRY utakuwepo Masjid Al Maamur.

Shughuli zote za maziko zitafanyika Masjid Al Maamur (kwa wanawake na wanaume).

Mwili wa Marehemu utaswaliwa baada ya Swalat Asr.

Marehemu ALHAJ SAID
EL MAAMRY ataenda kupumzishwa katika makaburi ya Kisutu baada ya Swalat Asr.

Mwenyezi Mungu ampe Mzee wetu mapumziko mema na amuweke pamoja na waja wema peponi, Ameen.

Manara: Sitokuwepo Kigoma, nitasali ili tushinde
Mwakingwe: Sina cha kuwadai wachezaji wangu