Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Selemani Jafo ametoa wiki mbili kwa mkandarasi Kampuni ya SUMA JKT pamoja Msimamizi Elekezi Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kuhakikisha wanakamilisha kazi ya kusiliba (plasta) kuta ambayo ilipaswa kuwa imekamilika.

Dkt. Jafo ametoa agizo hilo mara baada ya kukagua ujenzi wa jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais, unaoendelea katika eneo la Mtumba jijini Dodoma hii leo Februari 01, 2023 na kuonesha kutoridhishwa na kasi ya ujenzi wa jengo hilo, huku akimtaka mkandarasi kuongeza kasi.

Sehemu ya jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais ikiwa katika hatua ya ujenzi wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Selemani Jafo hii leo Februari 01, 2023.

Amesema, “Hapa mko nyuma sana wenzenu kule wako mbali sana kuliko ninyi na mara ya mwisho tulipokutana mkaniambia kazi itaenda kwa kasi lakini ndio mkaamua kabisa kusimama na mmeanza tena kufanya baada ya kusikia ninakuja kukagua, hapa naona hakuna userious katika kufanya hii kazi.”

Kwa mujibu wa mpango kazi uliowekwa, ujenzi huo upo nyuma kwa siku 41 hali inayotokana na kasi ya ujenzi wa jengo hilo kuwa ya kutoridhisha huku akisema pamoja na kuwa wameaminiwa na kupewa dhamana ya ujenzi wa jengo hilo la Serikali, lakini haijaonesha umakini katika utekelezaji wa mradi huo.

EWURA yatangaza ukomo wa bei ya mafuta
Aliyepotea kwa miaka 30 apatikana akiwa hai