Simba SC ina nafasi ya kurejea kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara hii leo iwapo itashinda dhidi ya Ndanda FC kutoka mkoani Mtwara.

Simba wanaikaribisha Ndanda leo katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakihitaji ushindi ili kuongoza ligi.

Kocha wa Wekundu hao wa Msimbazi, Mganda Jackson Mayanja amesema kwamba timu yake ipo vizuri baada ya maandalizi ya tangu Jumatatu wakiwa kambini nje kidogo ya mji ili wachezaji wapate utulivu.

“Tunatarajia mchezo mgumu na wenye ushindani mkubwa, lakini tumejiandaa kushinda,”amesema Mayanja.

Ikumbukwe Simba SC inaongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 48, baada ya kucheza mechi 21, ikiizidi pointi moja Azam FC iliyo nafasi ya tatu na ikizidwa kwa mbili na vinara, Yanga.

Vicent Bossou Atemwa Kikosi Cha Togo
Vijana 6 Wa Zenji Wa Shotokan Karate Kupigwa Msasa Dar es Salam