Wachezaji sita wa mchezo wa Shotokan Karate visiwani Zanzibar wamepata fursa ya kwenda kwenye Semina maalum na mashindano madogo ya mchezo huo ambayo yatafanyika jijini Dar es salam kuanzia tarehe 22 hadi 27 ya mwezi huu ambapo yatafanyika katika ukumbi wa Russia Culture jijini humo.

Akizungumza na Burudani Sensei Abdallah Hussein alisema kuwa wamepata mualiko huo ambapo vijana sita watapata fursa kwenda katika Semina hiyo.

“ Tumepata mualiko wa Mafunzo maalum ya mchezo wetu jijini dar es salam ambapo vijana wangu 6 watakwenda kwenye semina hiyo kisha watafanyiwa mitihani na mashindano madogo madogo”.

Semina hiyo itaongozwa na Sensei Jerome na Dula kutoka Tanzania wakishirikiana na Sensei Delmshal kutoka Afrika Kusini.

Simba Katika Mipango Ya Kurejea Kwenye Kilele Cha VPL
Sunderland Wamrejesha Emmanuel Eboue EPL