Uongozi wa Klabu ya Simba SC umetoa ufafanuzi wa kumpa mkataba wa Mwaka mmoja Mwaka mmoja Kocha Mkuu Mpya wa kikosi chao Zoran Manojlović, ambaye alitangaza jana Jumanne usiku (Juni 28).

Simba SC imemtangaza Kocha huyo kutoka nchini Serbia baada ya kuachana na Kocha Franco Pablo Martin mwishoni mwa mwezi uliopita, kufuatia kushindwa kukivusha kikosi cha Msimbazi kwenye hatua ya Nusu Fainali Kombe la Shirikisho ‘ASFC’.

Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally amesema, kabla ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja, Uongozi na Kocha huyo walikaa chini nakukubaliana, hivyo ni jambo la makubaliano ambalo limesababisha uwepo wa mkataba huo.

Amesema Mkataba aliosaini Kocha huyo ambaye amewahi kukinoa kikosi cha Al Hilal ya Sudan, una kipengele cha kuongezea mkataba mwingine endapo atafanikisha lengo alilowekewa na Uongozi wa Simba SC.

“Ni mwaka mmoja ambao utakua na nafasi ya kuongeza mwaka mwingine katika mkataba wake, haya yote ni kutokana na makubaliano ambayo pande mbili zimekubaliana, kwa hiyo ni jambo la kawaida sana.”

“Mashabiki wa Simba wanapaswa kufahamu huu ni utaratibu wa makubaliano na sio shinikiso kutoka upande mmoja, tunaimani kubwa kwa Kocha huyo, na kilichobaki ni kututhibitishia kwa vitendo kwa kazi yake ambayo itaanza mara moja baada ya kukabidhiwa rasmi kikosi.” Amesema Ahmed Ally.

Mbali na kukinoa kikosi cha Al Hilal ya Sudan kati ya mwaka 2020-21, Kocha Zoran pia amewahi kufanya kazi na klabu za      Primeiro de Agosto-Angola (2017–2019), Wydad AC-Morroco (2019–2020), CR Belouizdad-Algeria (2021) na Al-Tai-Saudi Arabia (2021).

Ahmed Ally: Kocha atawasili Dar mwezi Julai
Mataifa yahimizwa kulinda haki za wananchi