Mamlaka ya usimamizi wa ununuzi wa Umma imezitaka taasisi nunuzi kufuata utaratibu wa “Single Source” kwa ajili ya ujenzi na ununuzi wa vifaa katika miradi itakayotekelezwa ili kuharakisha utekelezaji wa Fedha za IMF zilizotolewa kwa ajili ya maendeleo na ustawi wa taifa.

Taarifa hii inakuja baada ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu kuelekeza kuwa fedha zilizopatikana kutoka IMF zitatumika kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo iliyoainishwa.

Katika uzinduzi wa Kampeni ya Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO-19 uliofanyika tarehe 10 Oktoba, 2021 jijini Dodoma, Rais Samia Suluhu aliagiza utaratibu wa “single Source” utumike kwa manunuzi yote ya umma.

Kupitia kwa Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu Injinia Mary Swai, Mamlaka imewakumbusha utaratibu wa ununuzi katika kazi za ujenzi, ununuzi wa huduma na bidhaa kwa njia ya “single source” unasimamiwa na Kanuni ya 159, 160 na 161 ya Kanuni za Ununuzi wa Umma, 2013 kama zilivyofanyiwa marekebisho na Tangazo la Serikali Na. 333. la 2016.

Katika kutekeleza maekelezo ya Mheshimiwa Rais, PPRA inawataka kuhakikisha wanapata wazabuni wenye sifa, uzoefu na uwezo wa kutekeleza mikataba hiyo kwa haraka na ndani ya muda wa mkataba na kuhakikisha Serikali inapata thamani ya fedha kwa manunuzi yote yatakayofanyika kuwa fedha zilizopatikana zinatakiwa kutumika ndani ya miezi tisa.

Majaliwa kaburini kwa Hayati Magufuli
Biashara United yasaka fedha za nauli ya Libya