Siwa ya Bunge la Nigeria imepatikana chini ya Barabara ya juu (flyover) Jijini Abuja baada ya kuokotwa na mwananchi aliyekuwa akipita maeneo hayo.

Watu wenye silaha walivamia Bunge la Nigeria na kuiba Siwa hiyo siku ya jana. Watu hao wanadaiwa kuongozwa na Mbunge ovie Omo-Agege ambaye amefungiwa kuhudhuria vikao hivyo.

Aidha, Msemaji wa Serikali amesema kuwa kitendo hicho ni uhaini na kinaashiria kuwa mtuhumiwa, Omo-Agege alikuwa akijaribu kupindua moja ya Mihimili ya Serikali ya Nigeria. Siwa ni ishara ya Mamlaka ya Bunge hilo na Sheria haziwezi kupitishwa bila kuwepo kwa kifaa hicho.

Licha ya kitendo hicho, Bunge liliendelea na kazi yake kwa kutumia Siwa ya ziada iliyokuwepo bungeni hapo ambapo kabla ya hapo Seneta wa Kaduna, Bwana Shehu Sani alivua mkanda wake na kuuweka sehemu ya Siha hiyo.

Hata hivyo, Chama tawala cha APC kimeita tukio hilo kuwa ni shambulio kwa demokrasia ya nchi hiyo na kutaka waliohusika kukamatwa. ambapo hadi sasa Seneta Omo- Agege anashikiliwa na Polisi akihusishwa moja kwa moja na tukio hilo

Al- Shabaab watishia usalama wa Walimu nchini Kenya
Video: Diamond na Nandy wakiwasili TCRA