Mabingwa mara tatu wa Fainali za Mataifa ya Afrika ‘AFCON’ Timu ya taifa ya Nigeria, wamefanya mabadiliko kwenye kikosi chao kuelekea Fainali hizo zitakazorindima nchini Cameroon kuanzia Januari 09.

Nigeria Imetwaa Ubingwa wa AFCON mwaka 1980, 1994 na 2013, itashiriki Fainali hizo kwa mara ya 20 mwaka huu 2022.

Sababu kubwa inayotajwa kwa Super Eagles kufanya mabadiliko kwenye kikosi chao ni Majeraha na kushindwa kufikia makubaliano na baadhi ya klabu zinazowamiliki wachezaji wa taifa hilo, walioitwa awali kwenye kikosi cha taifa hilo.

Victor Osimhen aliyepimwa na kuonekana ana Virusi vya Corona siku chache zilizopita na kuumia kwa Abdullahi Shehu kumesababisha mabadiliko katika orodha ya mwisho ya Super Eagles cha wachezaji 28.

Kukosekana kwa Osimhen na Henry Onyekuru anayecheza soka Ugiriki ambaye pia alikuwepo kwenye Fainali za AFCON 2019 zilizounguruma nchini Mirsi, huenda kukaathiri mipango ya benchi la ufundi la timu hiyo.

Kwa upande wa Walinda Lango haujaguswa lakini kulazimishwa kukaa karantini kwa Francis Uzoho anayecheza soka nchini Cyprus, sehemu ya ulinzi na kiungo, amemuongeza Tyrone Ebuehi anayecheza Serie A katika klabu ya Venezia, Italia.

Oluwasemilogo Ajayi amerejea katika kikosi baada ya beki wa kati Leon Balogun kupata jeraha na Ajayi pia anaweza kucheza kama kiungo.

Kikosi cha mwisho cha Nigeria ambacho kitashiriki Fainali za AFCON 2022 Makipa: Francis Uzoho (AC Omonia, Cyprus); John Noble (Enyimba FC); Daniel Akpeyi (Kaizer Chiefs, Afrika Kusini); Maduka Okoye (Sparta Rotterdam, Uholanzi).

Mabeki: Chidozie Awaziem (Alanyaspor FC, Uturuki); Kenneth Omeruo (CD Leganes, Spain); Oluwasemilogo Ajayi (West Bromwich Albion, England); William Ekong (Watford FC, England); Olaoluwa Aina (Torino FC, Italia); Jamilu Collins (SC Paderborn 07, Germany); Tyrone Ebuehi (Venezia FC, Italia); Zaidu Sanusi (FC Porto, Ureno); Olisa Ndah (Orlando Pirates, Afrika Kusini).

Viungo: Frank Onyeka (Brentford FC, England); Joseph Ayodele-Aribo (Glasgow Rangers, Scotland); Wilfred Ndidi (Leicester City, England); Chidera Ejuke (CSKA Moscow,Urusi); Kelechi Nwakali (SD Huesca, Hispania).

Washambuliaji: Ahmed Musa (Fatih Karagumruk, Uturuki); Samuel Chukwueze (Villarreal FC, Hispania); Henry Onyekuru (Olympiacos FC,Ugiriki); Moses Simon (FC Nantes,Ufaransa); Sadiq Umar (UD Almeria, Hispania); Taiwo Awoniyi (Union Berlin,Ujerumani), Odion Jude Ighalo (Al-Shabab Riyadh, Saudi Arabia); Alex Iwobi (Everton FC, England); Kelechi Iheanacho (Leicester City, England); Peter Olayinka (SK Slavia Praha, Jamhuri ya Czech).

Nigeria imeopangwa KUNDI D sambamba na mataifa ya Misri, Sudan na Guinea-Bissau.

Makundi mengine ya AFCON 2022
KUNDI A: Cameroon, Burkina Faso, Ethiopia na Cape Verde
KUNDI B: Senegal, Zimbabwe, Guinea na Malawi
KUNDI C: Morocco, Ghana, Comoros na Gabon
KUNDI E: Algeria, Sierra-Leone, Equatorial Guinea na Ivory Coast
KUNDI F: Tunisia, Mali, Mauritania na Gambia Morocco.

Simu za BlackBerry hazitatumika tena
Wakala wa Phiri afunguka dili la Young Africans