Wanamgambo wa Taliban wameanza oparesheni mpya ya kuwatafuta watu waliofanya kazi katika vikosi vya NATO na Serikali ya zamani ya Afghanistan.

Hayo yameelezwa kwenye waraka wa umoja wa mataifa kuwa Taliban wamekuwa wakienda nyumba kwa nyumba kuwatafuta wanaowalenga na kuzitishia familia zao.

Kundi hilo lenye msimamo mkali wa Kiislamu limejaribu kuwahakikishia Waafghanistan tangu lilipo twaa madaraka, na kuahidi hakutakuwa na kisasi, lakini kuna hofu kwamba Taliban wamebadilika kidogo tangu miaka ya ukatili ya 1990.

Onyo ambalo limetolewa kuhusu kundi hilo linalowalenga  washirika wa NATO na Serikali ya zamani ya Afghanistan limeletwa katika hati ya siri na Kituo cha RHIPTO cha Norway cha Uchambuzi ambacho hutoa usaidizi wa masuala ya ujasusi kwa Umoja wa Mataifa (UN).

“Kuna idadi kubwa ya watu ambao kwa sasa wanalengwa na Taliban na tishio liko wazi.”  Amesema Christian Nellemann, ambaye anaongoza jopo la walioandaa ripoti hiyo.

Nellemann amsema waraka umeandika kuwa wasipojisalimisha Taliban watawakamata na kuwashtaki, na kuwaadhibu wanafamilia kwa niaba ya watu hao.

Ameonya kuwa mtu yeyote ambaye yupo kwenye orodha ya Taliban yuko katika hatari kubwa, na kwamba kunaweza kuwa na mauaji ya watu wengi.

Mbowe majanga hayaishi
Tanzania Prisons yatema wachezaji 16