September 19, 2016 kituo cha TV cha CNN Kiliripoti kuhusu muigizaji mwenye mvuto wa kipekee kuanzia muonekano wake mpaka uigizaji wake, Angelina Jolie kufungua kesi ya kudai talaka kutoka kwa mume wake Brad Pitt, sababu zikilielezwa kuwa ni ndoa yao kukosa maelewano mazuri.
Kwa mujibu wa nyaraka za mahakama, wapenzi hawa walitengana kuanzia September 15, 2016, ikiwa ni miaka miwili na mwezi mmoja tangu walipofunga ndoa yao mnamo August 2014. imeelezwa kuwa Jolie anatafuta makazi mapya kwaajili ya kuishi na watoto wao sita huku akiiomba mahakama kumpa ruhusa Brad Pitt kuwatembelea watoto wake.
Inadaiwa pia Jolie ameiomba mahakama kumpa mamlaka ya kubakia na mali zote walizipata kwenye ndoa yao na suala la kugawana lifanyike siku za baadaye sana, ingawa pande zote mbili pia zimekubaliana kuhakikisha kuachana kwao kunakuwa kwa amani kabisa.
Akiongea na E! News jana Jumanne, Geyer Kosinski ambaye ni Meneja wa Jolie amesema kuwa Angelina yuko tayari kufanya jambo lolote ili kuwalinda watoto wake.
