Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), imehalalishiwa kiasi cha shilingi bilioni 38 ilichochukua kama kodi kutoka katika kampuni nya VIP Engineering and Marketing Ltd inayomiliwa na James Rugemalira baada ya Bodi ya Rufani ya Kodi za Mapato (Trab) kutupilia mbali maombi ya mmiliki huyo.

James Rugemalira

James Rugemalira

Trab imetupilia mbali kesi iliyofunguliwa na Rugemalira kupinga makato ya kiasi hicho cha fedha kilichochukuliwa na TRA ikitaka kirudishwe kwa madai kuwa kilikuwa kinyume na sheria. Kodi hiyo ilikatwa kupitia mkataba wa kuuza umeme kati ya kampuni hiyo na Pan African Power Solution (PAP), mwaka 2013.

“Mlalamikaji ameshindwa kupata marejesho kwa mwaka wa mapato 2013. Hivyo, hakuna uvunjivu wowote wa sheria uliofanywa na mlalamikiwa (TRA),” ilieleza sehemu ya maamuzi ya Trab.

VIP waliwasilisha rufaa hiyo Trab mwaka jana ambapo pamoja na mambo mengine waliitaka kutangaza kuwa TRA walifanya makosa katika usaili wa mapato ya kampuni hiyo katika biashara ya kuuza hisa zake zilizokuwa kwenye IPTL kwenda PAP.

Zlatan Ibrahimovic Kumalizana Na Man Utd Kesho
Arsenal Kuibomoa Leicester City, Wamtaka Riyad Mahrez