Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetoa elimu kwa wafanyabiashara na wadau mbalimbali walioshiriki Jukwaa la Fursa za Biashara mkoani Geita na kuwafafanulia juu ya masuala mbalimbali yanayohusu kodi.
 
Akizungumza katika Jukwaa hilo, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa mamlaka hiyo, Richard Kayombo amewataka wafanyabiashara wenye malimbikizo ya madeni ya kodi na wale wote waliokuwa wakifanya biashara bila kusajiliwa kuchangamkia msamaha.
 
“Nachukua fursa hii kutoa wito kwa wafanyabiashara wote wenye malimbikizo ya madeni ya kodi na wote waliokuwa wakifanya biashara bila kusajiliwa kuwasilisha maombi yao TRA ili waweze kupata msamaha huu wa riba na adhabu wa asilimia 100 ambapo mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 30 Novemba, 2018,”amesema Kayombo
 
Aidha, Kayombo amewahimiza wafanyabiashara wadogo waliopo kwenye utaratibu wa makadirio kusajiliwa na kupatiwa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) ambayo hutolewa na TRA bure bila ulazima wa kulipa kodi ya awamu ya kwanza.
 
  • Utafiti wa LHRC wabaini wafanyakazi wengi hawazijui haki zao
  • NEC yaujibu ubalozi wa Marekani, yautaka utoe uthibitisho
  • RC Brigedia Jenerali Nicodemas amgomea mkandarasi
 
Hata hivyo, Jukwaa la Fursa za Biashara limeandaliwa na Ofisi ya Mkoa wa Geita kwa kushirikiana na Shirika la Magazeti ya Serikali (TSN) ambapo Mamlaka ya Mapato Tanzania imeshiriki jukwaa hilo kwa ajili ya kutoa elimu ya kodi kwa wafanyabiashara na wadau mbalimbali hususani wa mkoani hapa
DC Ole Sabaya amsweka ndani mwekezaji shamba la Kibo
Thilo Kehrer ajiunga na mabingwa wa Ufaransa