Mshambuliaji wa kikosi cha Watford Troy Deeney, amethibitisha kurejea mazoezini baaada ya kufanya mazungumzo na ofisa wa Afya wa Serikali ya England.

Juma lililopita mshambuliaji huyo alisema hatarejea mazoezini mapema kutokana na hali ya mtoto wake mdogo, kwa kuhofia huenda akamuambukiza virusi vya Corona.

Hata hivyo Deeney amesema wakati akitoa kauli hiyo, watu walimuelewa tofauti na kuanza kumshambulia kupitia mitandao ya kijamii, lakini alikua anamaanisha tofauti na alivyoeleweka kwenye jamii.

“Nilisema sitarejea mazoezini wiki ya mwanzo wala sijasema kuwa sitorejea mazoezini kabisa watu walininukuu vibaya” Deeney

“Nimeongea na Dr Jonathan Van Tam makamu ofisa wa afya wa serikali na amekuwa mkweli”

“Amekuwa mwaminifu kwani amejibu maswali yangu na yale ambayo yalikuwa na ukakasi aliniweka wazi kuwa hana jibu” Deeney

“Amenihakikishia usalama kwa asilimia kubwa sana. Ameeleza kuwa kila kitu kitakuwa wazi na taarifa zitatolewa kwa haraka” Deeney

Bodi ya mikopo yatoa Sh 63.83 bilioni kwa wanafunzi
Boston Marathon 2020 Yafutwa

Comments

comments