Msanii wa muziki wa bongo fleva ambae anamiliki lebo ya Bilionea Kid, Rich Makovo amemjibu aliyekuwa meneja wake Sallam SK aliyedai kuwa bado wanamdai kwa kuwa walichokiwekeza juu yake hajakirudisha.

Rich Mavoko amesema kwa walipofikia sasa si vyema kuanza kuongeleana vibaya kikubwa ni kuheshimiana ameongezea kuwa WCB ilimkuta akiwa Brand tayari tofauti na wasanii wengine kama vile Rayvany, Harmonize na Lavalava.

“Unajua kwenye masuala ya kumzungumzia Rich Mavoko unazungumzia brand ambayo ilikuwepo, Kwahiyo uliichukua unataka kufanya nayo biashara, sasa unasema hajarudisha na huyo mwenye talent atakuwa amepata. Mimi sitaki kuongelea sana hivi vitu kwa undani, kila mtu anatakiwa kuheshimu kitu cha mwenzake kwanza halafu tuanze kuongeleana na kwenye kuongeleana vitu vibaya ni kutaka mtu kijitetea,”Amesema mavoko.

Hata hivyo Rich Mavoko amewaeleza mashabiki wake sababu ya kukaa kimya kwa kipindi chote cha vuguvugu la kuondoka lebo hiyo na kusema kuwa alikuwa kimya kutokana na mengi ambayo yalikuwa yanazungumzwa mtandaoni kuwa alikuwa ananyonywa na lebo hiyo, kitu kilichomfanya Mavoko kukaa kimya kwa muda katika tasnia ya muziki.

Aidha, Mavoko amedai kuwa kila mtu anatakiwa kumheshimu mwenzake huku akisisitiza huu sio muda wa kuanza kueleza nani alimkosea mwenzake.

 

Leo ni siku ya kutokunywa pombe duniani
Jambazi Sugu aliyetoroka jela kwa helikopta anaswa