Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya wanawake, Sebastian Nkoma amesema kuwa, anaamini akipata mechi ya mwisho ya kirafiki itakuwa kipimo kizuri kwaajili ya kikosi cha timu ya vijana kwenda kupambana na Nigeria ili kupata matokeo mazuri katika mchezo wa kwanza.

Amesema kuwa mpaka sasa vijana wake wameweza kucheza mchezo mmoja dhidi ya kikosi cha timu ya wakubwa ambao walitoka sare ya kufungana bao 1-1 ambapo ameongeza kuwa alikuwa na mpango wa kwenda Bukoba kwaajili ya mchezo mwingine lakini suala hilo halikuweza kufanikiwa

“Kambi tunaendelea vizuri na vijana wapo vizuri na katika ratiba zangu nilikuwa nimeanza kuweka mechi za kirafiki za hapa hapa nyumbani na zingine za kigeni kwa mfano ya hapa nyumbani nimeshacheza na timu ya wakubwa wao ile ya Twiga Stars na tuliweza kutoka sare ya bao 1-1, nilikuwa na mpango wa kwenda kucheza Bukoba lakini watoto wangu mpaka sasa hivi hawajapata hati za kusafiria, sasa tunaangalia uwezekano wa kuleta timu moja kutoka Kenya au nchi yoyote ya jirani na baada ya hapo tunaanza safari ya kwenda Nigeria, ” amesema Nkoma

Ameongeza, katika mchezo huo ambao ni wa raundi ya kwanza ya kuwania kufuzu fainali za kombe la Dunia watahakikisha wanacheza kwa umakini wa hali ya juu ugenini ili waweze kumalizia vizuri zaidi mechi ya nyumbani

Hata hivyo, iwapo Twiga Stars itaitoa Nigeria, itakutana na mshindi wa mechi baina ya timu za Morocco na Senegal ambapo mshindi wake ataingia raundi ya tatu ambayo itatoa timu mbili zitakazofuzu kombe la dunia litakalofanyika mwakani nchini Ufaransa

Mtatiro: Kenya ni taifa litakalokuwa mwalimu wa siasa na demokrasia duniani.
Kenyatta: Sikubaliani na uamuzi wa Mahakama lakini…