Mwenyekiti Kamati ya muda ya uongozi wa CUF, Julius Mtatiro amefunguka na kudai nchi ya Kenya imekuwa ikidharauliwa kwa kuwepo siasa za kikabila na watu wengi lakini leo hii imeweza kuishangaza dunia kwa kuweza kufuta matokeo ya urais.

Mtatiro ametumia ukurasa wake wa facebook kuzungumza hayo mara baada ya dakika chache taarifa kuzagaa juu ya uamuzi wa kesi ya uchaguzi wa rais nchini Kenya katika Mahakama ya Juu.

Kesi hiyo imeanza kusikilizwa rasmi tokea Agosti 26, 2017 baada ya Muungano wa vyama vya upinzani (NASA) kuishtaki Tume ya Uchaguzi (IEBC) kwa kile walichokidai tume hiyo ilifanya udanganyifu juu na kumpa ushindi Uhuru Kenyatta.

Mtatiro katika ukarasa wake Facebook ameandika haya; ”Kenya ni taifa tunalolidharau kwa sababu ya siasa na ukabila lakini Kenya ni taifa litakalokuwa mwalimu wa siasa na demokrasia duniani. Hata Marekani sasa watajifunza kupitia Kenya ”. ameandika Mtatiro.

”Mahakama ya juu Kenya imeamua kuwa Tume ya taifa uchaguzi Kenya iliendesha uchaguzi huo Kenya bila y akufuata Katiba”

”Mahakama imetoa mari kuwa ushindi wa Uhuru Kenyetta na Jubilee ni batili na imeufuta”#

”Mahakama imeiagiza IEBC kuitisha uchaguzi mw2ingine ndani ya siku 60”.

 

Amber Lulu akwamisha kazi mpya ya Young D
Twiga Star yaingia kambini, yaahidi makubwa Nigeria