Uongozi wa label ya King Cash unaosimamia kazi za rapa Young Dee, umesema umemchukulia hatua Amber Lulu na kumfikisha kituo cha Polisi baada ya kuvujisha picha chafu kinyume na makubaliano yao.

Kutokana na sakasaka hilo linaloendelea mitandaoni meneja wa King Cash amesema imewabidi kusitisha zoezi zima lilikouwa linaendelea lakuachia kazi mpya ya rapa Young Dar es salaam, mpaka upepo huo uliodhaniwa kuwa kiki kwa kazi mpya ya Young D upite.

”Tulikuwa tuachie wimbo mpya kama ambavyo tuliahidi lakini natangaza kwamba tumesitisha kuachia wimbo mpya kwa sababu ya haya mambo ambao yanaendelea mitandaoni. Sisi sio watu wa kiki, muziki wetu unatosha kuweza kutufanya muziki kuwa juu na sio mambo ya kiki,” alisema King Maarifa.

Ameeleza kuwa sitisho hilo ni kwa lengo la kupambana kupinga kauli ambazo zipo kwenye mitandao ya kijamii zikidai kuwa ilikuwa njia ya kufanya wimbo mpya ufanye vizuri mitandaoni.

Aliongeza, “Kwahiyo bado hatujapanga kuachia kazi mpya, bado Bongo Bahati Mbaya inafanya poa kila siku kwahiyo tuna nafasi ya kuendelea kusubiri hata baada ya miezi mitatu ili upepo utulie au siku yoyote mambo yakikaa sawa tutatoa lakini sio leo,”

Pia meneja huyo amewataka mashabiki wa muziki wa Young Dee kuendelea kumuamini rapa huyo huku akiwaahidi mambo mazuri hivi karibuni.

Magazeti ya Tanzania leo Septemba 2, 2017
Mtatiro: Kenya ni taifa litakalokuwa mwalimu wa siasa na demokrasia duniani.