Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa-UNHCR limesema kuwa wafadhili wake wako mbioni kuzuia msaada wa fedha kupelekwa nchini Uganda kufuatia tuhuma zilizowakumba maafisa wanaohudumia wakimbizi kuongeza idadi ya wakimbizi ili wapate fedha za ziada.

Aidha, uchunguzi wa kina bado unafanywa na serikali ya Uganda, Umoja wa Mataifa na Umoja wa Ulaya kuhusiana na tuhuma hizo, huku uchunguzi mwingine ukifanyika kwenye huduma ya chakula na vifaa vingine vya msaada kama viliwafikia wakimbizi  ama vilihongwa.

Hata hivyo, tayari wiki iliyopita serikali ya Uganda ilianza uchunguzi wa tuhuma hizo kwa maafisa wake kujihusisha na rushwa.

 

Video: Rais Magufuli asafiri nje ya nchi kushiriki mkutano wa wakuu wa nchi EAC
Mahakama yamfutia kesi ya madai Uhuru Kenyatta