Baada ya siku siku 10 za maombolezo tangu kifo cha malkia Elizabeth II kilichotokea, Septemba 8 huko Scotland, hatimaye Septemba 19, 2022 mwili wake umepumzishwa huku mazishi yake yakivuta hisia za watu wengi ulimwenguni huku taifa hilo la Uingereza likirejea kukabiliana na mgogoro wa kiuchumi na mabadiliko ya kisiasa.

Zaidi ya viongozi 100 wa dunia, akiwemo Rais wa Marekani Joe Biden na Mfalme Naruhito wa Japan walikusanyika jijini London, ambapo idadi kubwa ya watu ilihudhuria tangu kufanyika kwa mazishi ya Nelson Mandela mwaka 2013 nchini Afrika Kusini.

Elimu husaidia kupambana na athari za kiuchumi. Picha na UN.

Maziko hayo, yameonesha historia ya kifalme ya Uingereza, demokrasia ya kikatiba na Jumuiya yake ya Madola na beri lililobeba jeneza la malkia likiwa ni lile lililotumiwa wakati wa mazishi ya Malkia Victoria katika 1901, huku Waziri mkuu mpya wa Uingereza, Liz Truss na katibu mkuu wa Jumuiya ya Madola, Patricia Scotland wakisoma mistari ya Biblia.

Uingereza, sasa itarejea katika kuukabili mzozo mkubwa wa kiuchumi katika kizazi chake, uwepo wa hofu kuhusu fedha za umma nchini humo ikifanya pauni kufikia viwango vya chini zaidi dhidi ya dola tangu 1985 na kuendelea kuishi kwa ufalme wa mbali kukitia shaka huku nchi za Caribbean zikijadili iwapo zitamtupilia mbali mfalme kama mkuu wa nchi.

Wanawake waongoza tatizo la afya ya akili
Tozo hailengi kumpa mzigo Mwananchi: Mwigulu