Ujangili na Mauaji ya Tembo katika Hifadhi na Mbuga za Wanyama yamepungua kwa kiwango kikubwa kufuatia juhudi za Serikali kutumia vyombo vyote vya ulinzi na usalama kulinda wanyama.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof. Adopolf Mkenda wakati wa ufunguzi wa mkutano kwaajili ya kuwajengea uwezo vyombo vya ulinzi na usalama katika kukabiliana ujangili, ambapo amesema kuwa kiwango cha mauaji ya Tembo kimepungua kutoka Tembo 194 mwaka 2016 hadi kufika Tembo 23 mwezi Juni 2018.

Amesema kuwa katika kipindi hicho meno 211 na vipande 413 vya meno ya Tembo vilikamatwa, silaha 355 na risasi zaidi ya 20,000 zilizokuwa zinatumika na majangili zimekamatwa pia kwa ushirikiano na vyombo vya ulinzi na usalama wa maliasili.

“Ukikamata mhalifu anashtakiwa baada ya siku chache unakutana naye mtaani anatembea kifua mbele anaanza kukubeza, mambo kama haya yana punguza mori ya kufanya kazi, lazima vyombo vyote mshirikiane katika kupambana nao kikamilifu na majangili,” amesema Mkenda.

Aidha, vyombo hivyo ni pamoja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Mamlaka za Hifadhi za Taifa kwa udhamini wa Palms Foundation.

Hata hivyo amesema kuwa kuna changamoto kubwa katika suala la kukamatwa wahalifu na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria kwani wahalifu wakifikishwa mahakamani maranyingi huachiwa huru kwa kukosekana kwa ushahidi wa kuambatanisha ambao utawatia hatiani majagili na kupewa hukumu stahili.

Mkutano huo wa kujenga na kuongeza uwezo kwa vyombo vya ulinzi wa maliasili, umethibitishwa na Mkurugenzi msaidizi uzuiaji ujangili na Mwenyekiti wa kikosi kazi Taifa cha kuzuia na kupambana na ujangiri, Robert Mande, amesema wajumbe walioudhuria ni 136.

 

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Januari 24, 2019
Video: Kamishna mkuu TRA afunguka kuhusu wachimbaji wa madini

Comments

comments