Katibu Mkuu ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Waziri Mkuu, Bunge na Siasa, Uledi Mussa amesema atahakikisha michango ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya watumishi wa Ofisi hiyo inafikishwa kwa wakati.

Kiongozi huyo ametoa kauli hiyo leo jana juni 20 wakati akijibu maswali ya watumishi wa Ofisi hiyo mjini Dodoma katika  maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma inayoanzia Juni 16 hadi 23 ya kila mwaka.

Kila mwaka Tanzania imekuwa ikiungana na mataifa mengine ya Bara la Afrika kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma Barani Afrika  ambayo kauli mbiu ya mwaka huu ni‘ Uongozi wa Umma kwa Ukuaji Jumuishi,kuelekea katika Afrika tunayoitaka’.

“Nitafuatilia michango ya watumishi katika mifuko ya hifadhi ya jamii ili kuhakikisha inafika kama inavyotakiwa na kwa wakati ili hata wanapomaliza muda wao wa utumishi wasihangaike,” alisema Uledi

Katika hatua nyingine Uledi amewataka Wakuu wa Idara kuandaa  mpango wa mafunzo kwa watumishi na washirikishe kila mtu katika idara husika kabla ya kuuwasilisha kwake.

Katibu Mkuu aliyasema hayo wakati akijibu maswali ya baadhi ya watumishi wa ofisi hiyo, ambapo Anjani Ngulukia (Msaidizi wa Ofisi) alitaka kupatiwa ufanunuzi kuhusu suala la michango ya mifuko ya hifadhi ya jamii ambayo imekuwa haipelekwi kwa wakati.

Pia mtumishi mwingine Ernest Msabalala ambaye ni Mtunza Kumbukumbu Mkuu aliomba ofisi iandae utaratibu wa kuwa na mafunzo kwa watumishi ili kuongeza ufanisi wa kazi.

Kampeni ya "Let's Move!" Yamuingiza Michelle Obama Snapchat
CCM wazungumzia uamuzi wa wabunge wa Ukawa kutowasalimia