Vyombo vya Usalama nchini Urusi, vimetoa hati ya kukamatwa kwa mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu – ICC, Karim Khan ambaye mwezi Machi alitoa hati ya kukamatwa kwa rais wa Urusi Vladimir Putin kwa tuhuma za uhalifu wa kivita.

Mwendesha mashtaka huyo ambaye ni ambaye ni raia wa Uingereza na akihudumu katika mahakama ya uhalifu wa kivita yenye makao yake makuu The Hague, aliongezwa kwenye orodha ya watu wanaotakiwa na wizara ya mambo ya ndani, ya Urusi.

Aidha, Kamati ya Uchunguzi ya Urusi, ambayo inashughulikia uhalifu mkubwa, ilisema mwezi Machi kwamba Khan alikuwa anachunguzwa kwa kuaagiza mashtaka ya jinai kwa mtu ambaye kuwa hana hatia” – akimaanisha mashtaka ya uhalifu wa kivita dhidi ya Putin.

Hata hivyo, Mwendesha mashtaka wa ICC pia alikuwa anachunguzwa kwa madai ya kuandaa “shambulio dhidi ya mwakilishi wa taifa la kigeni ambalo lipo chini ya ulinzi wa kimataifa”, wachunguzi wa Urusi walisema wakati huo.

Kisarawe wavuka lengo upandaji miti Milioni 1.5
Mataifa 43 hatarini kuambukizwa kipindupindu