Kampuni ya simu za mikononi ya AIRTEL imezindua duka kwa ajili ya kutoa huduma kwa wateja wanaoishi katika maeneo mbali mbali ya mkoa wa Manyara huku vijana wakitakiwa kuchangamkia fursa za ajira zilizopo kupitia duka hilo.

Duka hilo limezinduliwa na Kamanda wa polisi mkoa wa Manyara, Fransic Masawe, ambaye amesema kuwa duka hilo litakuwa msaada mkubwa kwa wakazi wa mji wa Babati pamoja na maeneo jirani jambo ambalo amewataka vijana kutumia fursa hiyo kupata ajira kwa lengo lakujiongezea kipato.

Pia amesema huduma ya mawasiliano ni chachu ya maendeleo kwani inasaidia kutunza vitu muhimu hususani fedha ambazo watu wengi hutumia AIRTEL kwakufanya miamala pamoja na kupata mikopo.(Pause)

Naye Meneja wa AIRTEL mkoani Manyara, Peter Kimaro amesema duka hilo linalenga kusogeza hudumakaribu na jamii kwani kipindi cha nyuma wananchi walikuwa wanapata tabu kupata huduma za uhakika lakini pia hatua hiyo inatoa mwanya wakuongeza maduka katika maeneo ya mkoa huo ikiwemo wilaya  ya Kateshi.

Aidha, Amesema kua Kampuni hiyo inampango wakuongeza maduka mengine katika mkoa huo wa Manyara ili kuendelea kusogeza huduma zake kwa wateja kwa urahisi hususani katika maeneo ya vijijini.

Video: Majaliwa asema Dkt. Elly alitoa mchango mkubwa
Haji Ugando Kuitema Simba SC