Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Patrobas Katambi amemsweka ndani mwananchi mmoja mara baada ya kutaka kuvuruga mkutano wake na wananchi.

DC Katambi amechukua hatua hiyo wakati akizungumza na wananchi wa Wilaya hiyo kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero mbalimbali.

Ameseka kuwa serikali ya awamu ya tano ipo kwaajili ya kutatua kero za wananchi na kuwaomba kushirikiana kwa karibu na serikali.

“Serikali hii ipo kwaajili ya kuwatumikia wananchi na kutatua kero zinazowakabiri, hivyo akitokea mtu yeyote anataka kuvuruga na kuwafanya wananchi wasitoe kero zao lazima ashughulikiwe,”amesema DC Katambi

Jan Vertonghen kuimarisha mkataba wake Spurs
Joe Budden amrukia tena Eminem, ‘ntakupa kipigo’

Comments

comments