Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dkt. Athuman Kihamia amesema kuwa hakuna hasara yeyote inayosababishwa na chaguzi ndogo za marudio.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza Dar24 Media ambapo amesema kuwa chaguzi hizo zipo kisheria.

Amesema kuwa NEC inasimamia chaguzi hizo ndogo kisheria hivyo, haihusiki na suala la gharama inayotumika.

“Unajua NEC inasimamia chaguzi hizi zote kisheria, sisi hatuhusiki na masuala ya gharama, kimsingi tunacho kifanya ni kuweza kutimiza wajibu wetu,”amesema Dkt. Kihamia

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Oktoba 24, 2018
Paco Alcacer: Sijutii kuondoka FC Barcelona

Comments

comments