Rais wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli amefanya ukaguzi wa kushitukiza katika sehemu ya kukagulia mizigo na abiria upande wa Terminal (1) katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Rais Magufuli amefanya ziara hiyo leo October 5, 2016 mara baada ya kumuaga Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Joseph Kabila Kabange ambaye amemaliza ziara yake ya kiserikali ya siku tatu hapa nchini na kurejea nchini kwake.

Ziara ya Rais Magufuli uwanjani hapo ni mara ya pili ambapo awali mwezi Mei 2016 alitembelea kwa kushitukiza na kubaini kuwa mashine za ukaguzi (Scanners) zilikuwa hazifanyi kazi.

Katika ziara ya leo Rais Magufuli amebaini kuwa mashine hizo zinafanya kazi baada ya kujionea mwenyewe uhalisia wa namna mizigo inavyokaguliwa.

Rais Magufuli amemuagiza Mkurugenzi wa uwanja wa ndege wa Julius Nyerere, Paul Rwegasha kuwachukulia hatua za kinidhamu maafisa wawili walitoa taarifa za uongo pindi alipofanya ukaguzi wa kushitukiza mara ya kwanza.

“Walikuwa wawili walionidanyanya, alikuwa mmoja alisimama hapa na mwingine alikuwa huku. Leo waondoke na Muwaremote” – Rais Magufuli.

Video: Majaliwa aibana Magereza Dodoma, Mkuu wa mkoa apewa masaa kuchunguza
Video: Bodi ya wadhamini CUF yatua Mahakama Kuu