Rais wa Tanzania , Dk. John Pombe Magufuli amefanya ziara ya kushtukiza katika ofisi za Wizara ya maliasili na utalii (Mpingo House) kufuatilia utekelezaji wa Operesheni ya kukabiliana na ujangili inayofanywa na Kikosi Kazi kilichoundwa na wizara hiyo.

Akiwa Ofisini hapo Rais Magufuli amewapongeza sana kwa kazi nzuri askari waliopo katika Kikosi Kazi cha kudhibiti na kupambana na biashara haramu ya pembe za ndovu, ambapo amewakikishia kuwa anawaunga mkono na kuwataka wachape kazi, wawakamate wote wanaojihusisha na biashara haramu,

Rais Magufuli amesema hakuna wa kumbakiza, awe mkubwa au nani, wote wanaojihusisha na biashara haramu wakamatwe bila kujali cheo, umri, dini, kabila, wala umaarufu wako.

‘Hapa mmekamata pembe 50 maana yake tembo 25 wameuwawa, haiwezekani maliasili yetu ikawa inapotea hovyo hovyo kwa sababu ya watu wachache wenye tamaa ya kutaka utajiri wa haraka haraka‘ –Rais Magufuli

Video: DC Mjema atoa agizo kwa wafanyabiashara Ilala
Makonda awaasa wazazi kutowachagulia masomo wanafunzi