Meya wa halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob amekanusha taarifa zinazozagaa kuwa wapinzani wanatumikia Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kuweza kutekeleza majukumu yao.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam wakati akizungumza na Dar24 Media, ambapo amesema kuwa CCM wanatumia ujanja ujanja wa kutaka kudhoofisha upinzani.

Amesema kuwa wao kama wapinzani wanatekeleza Ilani yao kwani wana halmashauri 30 ambazo ni muhimu zaidi ya zingine ndio maana Katibu Muenezi Taifa wa CCM, Humphrey Polepole anafanya ziara ya kutembelea halmashauri zinatawaliwa na upinzani kwa nia ya kuzoofisha shughuli za maendeleo.

“Nimekuwa Meya wa Ubungo sijawa kuona Ilani ya CCM, na wala hakuna mtu wa CCM wala waziri aliyewahi kunilazimisha kutumia Ilani ya Chama hicho,”amesema Jacob

Basata yamjia juu Diamond, yadai ameitusi Serikali
‘Aliyefungia nyimbo za wasanii sio Shonza’

Comments

comments