Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imetoa tangazo kwa wanafunzi wote wanaotarajia kujiunga na masomo ya elimu ya juu kwa mwaka 2017/2018 kuwa maombi ya kujiunga na vyuo yatumwe moja kwa moja vyuoni.

Hayo yamezungumzwa  leo Julai 20 na Kaimu Katibu Mtendaji TCU, Profesa Eleuther Mwageni ambapo amesema hawatapokea maombi ya kujiunga na vyuo vikuu kama ambavyo ilikuwa miaka ya nyuma.

Aidha, ameeleza kuwa maombi ya kujiunga na elimu ya juu yatanza kupokelewa rasmi julai 22 kwenye vyuo vyote vya elimu ya juu.

Utaratibu huo umeanza rasmi mwaka huu mara baada ya wanafunzi wengi kuilalamikia Tume ya Vyuo vikuu Tanzania (TCU) kushindwa kufanya machaguo sahihi ya vyuo na taaluma zao, hivyo TCU imeamua kurudisha jukumu hilo kwa wanafunzi husika kufanya machaguo ya vyuo na taaluma wanavyotaka wao.

”Wanafunzi wenye sifa za kujiunga na vyuo vikuu wasisite kuchagua vyuo wanavyovipenda na kuhakikisha wanakuwa makini na programu zilizowekwa na vyuo iwapo zinatambuliwa na Tume” amesema Eliuther Mwageni.

Amesema TCU haitatoza ada yeyote ya udahili kwa waombaji

Video: JPM awataka Warundi wote warudi kwao
Video: Tutawashughulikia wote wanaotoa matamshi ya kichochezi - Majaliwa