Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amepokea michango yenye thamani ya sh. milioni 660.25 zikiwa ni fedha taslimu, hundi na vifaa mbalimbali kwa ajili ya wananchi walioathirika na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera, mwezi uliopita.

Majaliwa amepokea michango hiyo leo Oktoba 11, 2016 kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es Salaam. Waliokabidhi misaada hiyo ni Makamu wa Rais wa kampuni ya ACACIA, Deodatus Mwanyika wametoa sh. milioni 325 ambazo tayari wameshaziingiza kwenye akaunti ya maafa, Balozi wa Japan nchini, Masaharu Yoshinda pamoja na Shirika la Misaada la Maendeleo la Japan (JICA) ambao wametoa vifaa vyenye thamani ya sh. milioni 220, Mkurugenzi Mkuu wa TBC1, Dk. Ayoub Rioba ambaye alikabidhi hundi za sh. milioni 41.55. Bofya hapa kutazama video

Neil Warnock Amnusuru Marouane Chamakh
Jurgen Klopp Aendelea Kupokea Taarifa Za Majanga