Meneja wa majogoo wa jiji Liverpool Jurgen Klopp, ameendelea kupokea taarifa za majanga kuhusu kikosi chake ambacho mwanzoni mwa juma lijalo kitakabiliwa na mpambano wa kukata na shoka dhidi ya Manchester United.

Mapema hii leo meneja huyo kutoka nchini Ujerumani, alipokea taarifa za kuumia kwa kiungo mshambuliaji kutoka nchini Uholanzi Georginio Wijnaldum alipokua kwenye jukumu la timu ya taifa lake usiku wa kuamkia hii leo, lakini muda mchache uliopita jopo la matabibu wa Liverpool limemueleza kuhusu maendeleo ya mshambuliaji wa pembeni Adam David Lallana.

Taarifa za Lallana zinaeleza kuwa, huenda akaukosa mchezo dhidi ya Man Utd, kutokana na hali ya jeraha kutoridhisha mpaka hivi sasa.

Mshambuliaji huyo wa pembeni kutoka nchini Uingereza, alipata maumivu ya misuli ya paja wakati wa mchezo wa ligi dhidi ya Swansea FC ambapo Liverpool walichomoza na ushindi wa mabao mawili kwa moja.

Video: Waziri Mkuu apokea michango ya sh. mil. 660, tetemeko Kagera
Picha: Luis Suarez Achukua Jukumu La Kulinda Lango