Wanafamilia wa Vijana 21 waliofariki katika mazingira ya kutatanisha katika baa moja huko London mashariki nchini Afrika Kusini, wamekusanyika kwa pamoja kwa kuwahusisha Viongozi wa jumuiya kufanya ibada ya maombi.

Hatua hiyo, inafuatia kutokana na msiba huo ulioacha maswali, baada ya Vijana hao wengi wakiwa wa umri kati ya miaka 13 hadi 18, kukutwa wamekufa ndani ya baa moja maarufu katika jiji hilo la kusini mwa London Mashariki.

Chanzo kamili cha vifo hicho bado hakijathibitishwa, lakini baadhi ya mashuhuda wamesema kulitokea harufu kali iliyosababisha kukosekana kwa hewa safi iliyoenea katika jengo hilo usiku wa mkasa huo.

Baadhi ya waathiriwa wa tukio hilo waliolazwa hospitalini, wamesema bado wana maumivu ya mgongo, kutapika na vifua kubana, huku Polisi ikisema bado inaendelea na uchunguzi katika kitongojini hicho kwa ajili ya kupata ushahidi kamili.

Wanafunzi hao, walifariki wakiwa katika sherehe ya kumaliza Mitihani yao, ambapo baadhi walifia hospitalini baadaye, huku wakiwa hawana dalili zozote za kuumia.

Makundi ya watoto yapotezana na wazazi wao
Hewa ya sumu yaua 13, zaidi ya 250 wajeruhiwa