Vijana Mkoani Njombe wametakiwa kuungana na kuanzisha vikundi vya ujasiliamali ili kupambana na umasikini pamoja na kukabiliana na changamoto ya ajira.

Ushauri huo umetolewa na Mwenyekiti wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Njombe, Nehemia Tweve ambapo amesema kuwa Serikali ina mpango madhubuti wa kuhakikisha inawakwamua Vijana kutoka katika umasikini kwa kuunda vikundi.

“Hakuna Fedha itakayotolewa kwa mtu mmoja mmoja ni lazima tuzingatie suala la vikundi, unganeni muwe watu hata zaidi ya watano mnatosha kuanza shughuli mnayoitaka kwa ajili ya kujiajiri,” amesema Tweve.

Ameongeza kuwa halmashauri zote nchini zimeagizwa kutenga asilimia kumi ya mapato ya ndani ambapo kati ya hizo tano ni kwa ajili ya kukopeshwa Vijana.

Hata hivyo, ameongeza kuwa Vijana wanatakiwa kujiimarisha kwa kupambana na umasikini kwa vitendo na sio maneno.

 

Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Aprili 17, 2018
Mkojo wa Sungura wageuka dili mkoani Njombe

Comments

comments