Wanawake viongozi wa nchi na serikali, wamekutana kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa nje ya mjadala mkuu wa Baraza, kuzungumzia nafasi muhimu ya uongozi wa wanawake kwenye utatuzi wa changamoto zinazoikabili dunia, sambamba na kujenga mustakabali endelevu.

Taarifa iliyotolewa hii leo, jiijni New York, Marekani na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kushughulikia masuala ya wanawake, UN Women imesema wanawake hao wakuu wa nchi na serikali wamekutana kupitia jukwaa jipya la Wanawake viongozi, la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA, lililoanzishwa 2021.

Katika mkutano huo, wenye maudhui na majawabu ya mabadiliko kutoka kwa wanawake viongozi kwa changamoto za sasa zinazohusiana, umeonesha ushiriki kamilifu na ufanisi wa wanawake kwenye siasa kuweka lengo la kupitia maamuzi muhimu na kushughulikia vipaumbele vya dunia kwa ufanisi na ujumuishi.

Vikao vya akina mama kujadili migogoro ya kifamilia huwasaidia kupata mbinu za kuepuka majanga yanayoweza kujitokeza. Picha na UN.

Miongoni mwa waliohudhuria mkutano huo, andaliwa na Ofisi ya Rais wa Baraza Kuu la UN pamoja na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kushughulikia masual ya wanawake, UN Women kwa ushirikiano na Baraza la wanawake viongozi, CWWL ni pamoja na Rais Novák wa Hungary, Waziri Mkuu wa Bangladesh, Sheikh Hasina,

Wengine ni Waziri Mkuu wa Aruba, Evelyn Wever-Croes of Aruba, Waziri Mkuu wa St. Maarten, Silveria E. Jacobs na Waziri Mkuu wa zamani wa New Zealand, Helen Clark, Waziri Mkuu wa Iceland, Katrín Jakobsdóttir, Waziri Mkuu wa Samoa, Fiamē Naomi Mataʻafa na Waziri Mkuu wa Uganda, Robinah Nabbanja.

Mikoa yenye viashiria vya kigaidi yatajwa
Mkurugenzi wa Michezo azishauri Simba SC, Young Africans