Idadi ya Wabunge wengi nchini Somalia, imeidhinisha Baraza jipya la mawaziri lililoteuliwa nchini humo na kuipa nguvu Serikali ya Waziri Mkuu, Hamza Abdi Barre yenye wanachama 75 ikiwa ni muda mfupi baada ya makombora kushambulia vitongoji vya makazi karibu na ikulu ya rais huko Mogadishu.

Spika wa Bunge la Somalia, Adan Mohamed Nuur Madobe amesema, “Idadi ni wabunge 237, wabunge saba walikataa, mbunge mmoja alijizuia huku baadhi ya wabunge 229 wakiidhinisha idhini ya mawaziri wapya, kwa hivyo imeidhinishwa.”

Katika kura hizo zilizopigwa kwa kunyoosha mkono Agosti 7, 2022 hakukuwa na madai ya mara moja ya kuhusika na shambulio hilo, ingawa changamoto za usalama inasalia katika ajenda ya Baraza la Mawaziri ambalo limeteuliwa hivi karibuni.

Baraza hilo la mawaziri, ambalo linamjumuisha Naibu Kiongozi wa zamani wa Al-Shabaab, Mukhtar Robow, ambaye pia linajulikana kama Abu Mansur aliyeapishwa kuwa Waziri wa masuala ya Dini nchini humo.

Waziri Mkuu, Hamza Abdi Barre akiongea baada ya matokeo ya kura amesema, “Namshukuru Mwenyezi Mungu na nimefurahishwa sana kwamba Wabunge waliidhinisha kwa kauli moja Serikali yangu na mpango wake wa utatekelezwa, Mwenyezi Mungu akipenda.”

Mbali na waasi wa Al-Shabaab, ambao wamekuwa wakiendesha vita vya umwagaji damu dhidi ya Serikali na watu wa Somalia kwa miaka 15, tishio la ujio wa baala la njaa pia itakuwa moja ya kipaumbele cha Baraza jipya la Mawaziri.

Kabla ya mzozo wa Urusi na Ukraine, Somalia iliagiza asilimia 90 ya ngano yake kutoka nchi zote mbili, huku akiba ya chakula inayotolewa na wafadhili wa kimataifa ikiwa ikipungua mjini Mogadishu.

Akizungumzia masuala ya kiusalama, Rais wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamoud amesema, ili kukomesha uasi huo kunahitaji zaidi ya mbinu za kijeshi na kwamba umoja na upendo vitasaidia kupunguza hali iliyopo.

PPRA yafunguka fursa zaidi ya sh. 6 trilioni kwa makundi maalum
Mashambulizi yauwa 20, Vijiji viwili vikitekwa