Upinzani wa mrengo wa kulia nchini Hispania, umepinga hatua ya Serikali ya nchi hiyo ya kutaka kuondoa kipengele cha uchochezi kama mashtaka hatua ambayo inakuwa wakati joto la Jimbo la Catalunya lililokuwa linataka kujitenga na Uhispania likiwa bado halijasahaulika.

Wapinzani hao wa chama cha Popular Party na kile cha Vox Party vinasema hatua hiyo itakuwa ni kama zawadi kwa vyama vinavyotaka kujitenga, na ni kwa ajili ya serikali kupata uungwaji mkono bungeni.

Maandamano ya Wananchi mbele ya Bunge la Uhispania. Picha ya Reuters.

Mapema hapo jana, (Novemba 25, 2022), Bunge la nchi hiyo liliidhinisha muswada wa kufanyia mabadiliko sheria ya uhalifu kwa ajili ya kuondoa kile kinachoonekana na serikali ya mrengo wa kushoto ya Uhispania, kama sheria ya zamani na kuibadilisha na sheria inayoambatana na maadili ya kisasa ya Ulaya.

Mabadiliko hayo, yanatarajiwa kabla ya mwisho wa mwaka huu na Mashtaka ya uchochezi ndiyo yaliyokuwa yamefunguliwa dhidi ya kiongozi wa zamani wa Catalunya, Carles Puigdemont, na wenzake na kuwapelekea kuihama nchi hiyo wakihofia kifungo jela.

Tanzania mjumbe Kamati kuu Wanyamapori, Mimea
Wafanyakazi TRA warudisha kwa jamii Katavi