Wakala wa mshambuliaji wa pembeni wa Real Madrid Gareth Bale, amesema mchezaji wake anataka aendelee kubakia klabuni hapo, na haitaji kurudi EPL.

Bale amekua anahusishwa na mpango wa kurejea katika ligi ya England (EPL) huku klabu yake ya zamani Tottenham Hotspur na Manchester United zikitajwa kumuwania.

Winga huyo raia wa Wales mwenye miaka 30 siku za hivi karibuni alikuwa anahusishwa kurudi EPL baada ya kutokuwa kwenye maelewano mazuri na kocha wake Zinedine Zidane.

Bale ilibakia kidogo tu ajiunge na timu mojawapo ya China msimu uliopita baada ya sintofahamu kunako klabu ya mabingwa mara nyingi zaidi wa ligi ya mabingwa Ulaya (UEFA – 13).

Akizungumzia kuhusiana na tetesi hizo amesema “Sifikiria kama hilo linaweza kutokea kipindi hiki, licha ya kushinda karibia kila timu Madrid bado anaonekana kuwa na furaha”. Alisema Jonathan Barnett (wakala wa Bale)

“Kurudi EPL itakuwa ni jambo kubwa kwa sababu ya aina ya maisha anayoisha hapa, Hana tamaa ya fedha kama wengine hivyo sioni kama hilo linaweza kutokea”.

Tangu ajiunge na Real Madrid kwa rekodi ya aina yake mwaka 2013 Gareth Bale ameshinda mataji kama ligi ya mabingwa mara nne, La Liga, Copa del Rey, Kombe la Dunia ngazi ya vilabu, na Kombe la ligi ya Hispania yote mara moja, na Uefa Super mara tatu.

Hitimana Thierry aweka pembeni usajili
Membe aachwa pekeyake Jahazi za wakosaji CCM, Kinana akiomba radhi