Jeshi la polisi Kanda maalumu ya Dar es salaam  liwametaka wananchi kuwa makini kuepukana na matapeli ambao kwa sasa wanakuja na mitindo tofauti tofauti ya kufanikisha adhma yao ya utapeli.

Mapema leo akizungumza na wanahabari Kamanda wa polisi Kanda maalumu Simon N. Sirro amesema kumekuwepo na malalamiko ya utapeli wa magari ambao unaendelea kwa sasa na kwamba kwa nyakati tofauti malalamiko ya kukodisha gari na kutapeliwa yamefikishwa kituoni.

Kamanda Sirro amesema kwa sasa tayari kuna watuhumiwa wawili wa matukio tofauti ambao ni Tumsifu Kyondo anayetuhumiwa kukodisha gari ya Bw. Aufuro Moshi Mkazi wa Mlimani City aina ya Toyota Noah kwa lengo la kutumia kwenye sherehe na kutokomea nalo  machi mwaka huu na kuja kulikamata machi 15 kwa Bw. Rashid Mohamed mitaa ya kinondoni na kudai aliuziwa na Bw. Kyondo.

Pia amemtaja Ally Salehe mtuhumiwa wa tukio lingine tofauti kuwa alikiuka makubaliano waliyojiwekea na Bw. Clif George ambapo alikabidhiwa gari la Toyota Harrier  no. T.468CC kwa makubaliano ya kulipa milioni 18 hatimaye mtuhumiwa huyo alikimbia na gari hilo  Mpaka alipokuja kukamatwa na juni 02 akiwa na gari hilo.

Hata hivyo kamanda Sirro amesema upelelezi bado unaendelea na watuhumiwa watafikishwa mahakamani mapema pindi utakapokamilika, huku akisisitiza wamiliki wa magari na waendeshaji wanapaswa kuwa makini ili kuepuka matapeli na kutoa taarifa pindi waonapo hali kama hizo zinazotia hofu ya utapeli.

Eid Mubarak
SERIKALI YASHAULIWA KUFUNGIA WAGANGA FEKI