Serikali imeshauriwa kuwafungia waganga wote wenye vituo vya tiba asili ambao hawana vigezo vya kutibu magonjwa mbalimbali kwa kutumia miti shamba na kupelekea matatizo makubwa kwa jamii.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Baraza waganga watafiti tiba asili wa halmashauli ya wilaya kinondoni, Maxmilian Lyana alipokua akiongea na Dar24 ofisini kwake tandale sokoni jijini Dar es salaam.

Aidha, Lyana aliongeza kuwa kuna utapeli mwingi kupitia tasnia hiyo ya tiba asili hivyo kuisababisha kudharaulika na kutokuheshimika kwa wateja wao ’’Watu lazima waelimishwe kuhusu waganga wa tiba asili, kwa maana wapo wanaosema kuwa uganga ni uchawi’’alisema, Lyana.

Kwa upande wao wanainchi waliofanya mahojiano na Dar24 walitoa maoni tofautitofauti,  wengine wakisema waganga wengi wa tiba asili wa sasa ni matapeli hivyo wanawaibia wanainchi na  kuwasababishia matatizo makubwa.na wengine walikiri kusaidiwa na tiba hizo za asili.

Hata hivyo wanainchi wameiomba serikali kusimamia ipasavyo tasnia hiyo ambayo ni kiungo mhimu sana kwa afya za binadamu na kuhakikisha waganga wote feki wanakamatwa ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza.

Wamiliki wa Magari Watahadharishwa na Utapeli Dar.
Video: Kamanda Sirro ampongeza Mwanamke shujaa, Ulinzi wakutosha Eid el Fitr