Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka mawakili wote wa serikali kufanya kazi kwa bidii pamoja na kutekeleza majukumu kwa kuzingatia kanuni, ili kuepuka migogoro.

Waziri Mkuu ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa mafunzo kwa  mawakili wa serikali ikiwa ni maadhimisho ya miaka mitano ya ofisi ya wakili mkuu wa serikali yaliyofanyika katika ukumbi wa jakaya Kikwete   Jijini Dodoma na kuzitaka taasisi zote za serikali kutoa ushirikiano kwa ofisi ya wakili mkuu wa serikali.

Amesema, “hakikisheni mfumo wa kieletronic unatumika ili kuhakikisha serikali inaimarisha sekta ya uchumi,  Serikali itaendelea kutenga bajeti kwa ajili ya ofisi hii na kutoa ushirikiano hivyo wakili mkuu wa serikali kaa mkao wa kula kwani serikali iko nyuma yenu kuhakukisha kila kitu kinakuwa sawa.”

Kwa upande wake Waziri wa katiba na sheria, Dkt. Damas Ndumbaro amesema ofisi ya wakili Mkuu wa serikali kwa miaka 5 wameweza kumaliza mashauri mengi kwa njia ya ushuluhishi pamoja na amani na kufanikiwa kuokoa fedha ambazo serikali ingelazimika kulipa na ingeshindwa katika kesi hiyo.

“Mashauri 65 na kwa usuluhishi mashauri 7 na katika mashauri hayo yote tumeweza kuikolea serikali shilingi Trilioni 7.5,” amesema Dkt.Ndumbaro huku Wakili Mkuu wa Serikali, Boniphace Luhende  akisema mafunzo hayo yataleta uandaaji wa mikataba pamoja na utatuzi wa migogoro mbalimbali.

Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali imeongeza uwanda wa utoaji huduma katika mikoa 17 kwa kufungua ofisi za masijala na maadhimisho hayo yamebeba Kauli mbiu isemayo, “Miaka mitano ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali,Tulipotoka,Tulipo na Tunapoelekea.”

Rais Samia aipongeza Young Africans Ikulu
The Gunners wamkomalia Joao Cancelo