Washika Bunduki wa Kaskazini mwa jijini London ‘Arsenal’ wameanza mawasiliano na beki wa Manchester City, Joao Cancelo kwa mujibu wa ripoti baada ya mkopo wake kumalizika FC Bayern Munich.

Arsenal imeonyesha nia ya kumsajili kwa sababu hatima yake Man City bado haiweleweki kwa hiyo wanataka kujaribu bahati yao dirisha hili la usajili.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Fabrizio Romano, Arsenal imeonyesha imevutiwa na beki huyo wa kimataifa wa Ureno.

Arsenal iliwasiliana na wakala wa beki huyo na kutokana na uhusiano mzuri waliokuwa nao huenda mambo yakaenda sawa kwa upande wao.

Cancelo alijiunga na Bayern kwa mkopo katika dirisha dogo la kiangazi kutokana na ukweli kwamba Pep Guardiola hakuonyesha kumuhitaji.

Imeelezwa beki huyo hana mpango wa kukipiga Man City na atajipanga akatafute maisha sehemu nyingi huku Arsenal ikihusishwa.

Arsenal inataka kuimarisha safu yake ya ulinzi baada kuzingua dakika za mwisho katika mbio za kuwania ubingwa.

Watendaji Serikalini waaswa kuzingatia Sheria
Ancelotti atia presha usajili wa Harry Kane