Watumishi wa afya wa kutoa huduma za usingizi wanahitajika zaidi nchini ili kuweza kutoa huduma hiyo kwa wingi na ukaribu zaidi mara zinapohitajika kwa wagonjwa wanaohitaji upasuaji kwa usalama katika hospitali.
 
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Idara kuu ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya wakati wa ufunguzi wa Mtaala wa kufundishia watu watakaotoka na Shahada ya Huduma ya Usingizi itakayotolewa na Chuo Cha Afya na Sayansi Shirikishi MUHAS leo jijini Dar es salaam.
 
Dkt. Ulisubisya amesema kuwa kabla ya mtaala huo kupitishwa hapo nyuma wagonjwa walikuwa wanapata huduma za usingizi pindi wanapohitaji kufanyiwa upasuaji kutoka kwa wataalamu waliopata mafunzo kwa mwaka mmoja au waliojifunza kwenye sehemu zao za kazi.
 
“Nawaagiza wenzetu wa MUHAS wahakikishe kasi ya kuandaa mtaala wa kufundishia iongezwe na uletwe haraka ili kuweza kupata wataalamu wa kutoa huduma za usingizi ili wakafanye kjazi kwenye Hospitali za Rufaa za Mkoa” amesema Dkt. Ulisubisya.
 
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mafunzo wa Shahada za Mwanzo MUHAS, Prof. Mainem Moshi amesema kuwa tayari wameshapeleka mtaala na vifaa tiba kwani wanahitajika takribani wahandisi elfu 8 nchini.
 
  • Diwani alalamikia kundi la Fisi
  • LIVE: JPM akizindua Hati ya kusafiria ya Kielektroniki
  • 500 ya nembo yawafukuzisha kazi walimu watatu
 
Hata hivyo, Prof. Mainem amesema kuwa kusimamishwa kwa mtaala wa kufundishia shahada ya udhamiri kwa kozi za ukunga kumepelekea vifo 556.

Mutungi aingilia kati kampeni za uchaguzi Siha, Kinondoni
Alama za vidole sasa kusajili laini za simu