Watoto 15 nchini Sudan Kusini wameripotiwa kufariki dunia kutokana na makosa yaliyofanywa wakati wa utekelezaji wa programu ya kutoa chanjo ya surua.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Serikali ya nchi hiyo iliyotolewa na Waziri wa Afya, Riek Gai Kok wafanyakazi waliotekeleza program hiyo katika jimbo la Mashariki Ikweta hawakuwa na vigezo na hawakupata mafunzo maalum, hivyo walitumia sindano zisizo na usafi kuchanja waototo.

Hiyo sio mara ya kwanza kwa makosa ya kutumia sindano zisizo salama katika zoezi la kuchanja watoto. Huduma za afya zimeendelea kusuasua katika nchi hiyo tangu mwaka 2013 ilipotoka kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Serikali imeeleza kuwa watoto hao wamefariki katika zoezi hilo lenye lengo la kutoa chanjo kwa watoto wa chini ya umri wa miaka 5, na takribani watoto milioni mbili wanapaswa kupatiwa chanjo hiyo muhimu.

Marekani yaigeuzia ubao China, yatoa onyo kali
Kibiti yatakiwa kudumisha amani